HESLB, Maafisa Wa Mikopo (loan officers) kukutana na Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu. 

Maafisa mikopo zaidi ya 80 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu (HLIs) nchini watakuwa na kikao kazi cha siku mbili ili kuboresha huduma za utoaji wa mikopo kwa wanufaika wanaoendelea na masomo.

Kikao hicho cha siku mbili kitafanyika leo tarehe 16 na 17 Machi 2017 katika Chuo Kikuu Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Dkt. Cosmas Mwaisobwa ambaye anaratibu kikao hicho, amesema kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka, kinalenga kuwapa maafisa mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu mikakati mipya ya jinsi ya kusimamia madawati ya mikopo kulingana na mabadiliko ya kimifumo na kiutendaji kuhusiana na utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Kikao hicho pia kitatumika kama njia ya kupokea mrejesho wa maafisa mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa watendaji wa Bodi ya Mikopo.

             heslb, ©2017.                                                        

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s