Fahamu mambo muhimu unapokuwa ni kiongozi.

1. Kuwasilikiza unaowaongoza:  Mtu anapokuwa ni kiongozi Wa kundi Fulani, amepewa dhamana ya kwa niaba ya watu wake. Hii haimaanishi kuwa wewe ni maridadi sana au mwenye akili sana kuliko watu watu wako, La hasha. Watu unaowaongoza wanao uwezo mabalimbali na mkubwa tena pengine kuliko wewe, pia wanayo mawazo yenye tija juu ya kundi lao. Unapokuwa ni kiongozi sasa yakupasa kuwasikikiza sana watu wako kwa maana  mawazo yao ndiyo yatakayo kusaidia wewe katika uongozi wako.

2. Nidhamu: Ni jambo la msingi sana  kwa kiongozi yeyote kuwa na maadili katika jamii na pia katika mazingira yake ya kazi. Watu wanapokuona wewe kama kiongozi Mara nyingi hutegemea mambo makubwa sana tena zaidia ya hata ambavyo wewe ungeweza kufikria kuwa wanayofikria na kuyategemea kutoka kwako. Unapokuwa na matendo mengi yasiyo maana (mabaya) watu wengi hupoteza imani kwako hivyo kukudharahu kwa kiasi kikubwa. Na sasa hawatakueshimu tena kwani wamekufanya kama wewe kuwa mtu wa chini sana. Na lolote utakalolisema wewe hawatalitilia maanani.

3. Msimamo:  Kuwa na kile unachokiamini na kukisimamia ipasavyo. Jambo linalowafanya viongozi wekwa kuwa na sifa nyingi kama  Mwl Nyerere, Mandela, Kinjikitile Ngwale na wengine wengi huwa ni kile kitu walichokisimamia kwa katika uongozi wao, kiongozi unapokuwa na msimamo legelege watu wanaokuamini hupoteza imani na wewe pia mambo yale unaliyoyapanga uongozini hayatatimia (fanikiwa). Mara nyingi watu wanaweza kutoelewa vizuri au kuchanganya hata mambo haya msimamo na kuwasikiliza watu (demokrasia). Ni vema sana kuwasikikiza lakini si kuyumbishwa na mawazo yasiyojenga.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: